Dar es Salaam. Mwandishi wa habari wa TV 3, Gwamaka Francis Gehas, ambaye alidaiwa kutoweka tangu Januari 3, 2025, amepatikana akiwa nyumbani kwa shangazi yake katika eneo la Kitunda.
Kulingana na taarifa kutoka kwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, baada ya ufuatiliaji wa kina, jana Januari 5, Makao Makuu ya Polisi Dodoma walipata habari za kuaminika zikionyesha kuwa Gwamaka alikuwa Kitunda.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili, lengo likiwa ni kupata maelezo ya Gwamaka ili kubaini chanzo cha kutoweka kwake na hali yake katika kipindi hicho.
“Uchunguzi huu utatusaidia kuelewa ikiwa kuna jambo lolote la siri nyuma ya hali hii, na hatua stahiki zitachukuliwa kulingana na ushahidi utakaopatikana,” imesema taarifa hiyo.
Endelea kufuatilia ECNETNews kwa habari zaidi.