Texas, Marekani
Baada ya kipindi cha kimya, mwongozaji na mwigizaji maarufu kutoka Houston, Texas, Alenga Elize, anayejulikana kama Alenga The Great, amezindua sinema yake mpya ya Kiswahili iitwayo ‘Lost Love (Wolf In a Sheep’s Clothes).’
Alenga The Great amejidhihirisha kama kiongozi katika tasnia ya filamu kwa kuwasilisha hadithi zinazokonga moyo, akicheza jukumu muhimu katika kuendeleza tasnia ya Bondowood Movie.
Alenga The Great ameelezea kuwa filamu hiyo imeweza kutazamwa na maelfu ya watu katika muda mfupi, akipongeza mchango wa timu yake ya Izack Productions na waigizaji walioshiriki. Filamu hii inatoa hadithi zenye maudhui ya Kiafrika, zikiwa na visa vya kusisimua, mapenzi ya dhati na usaliti, na inashauriwa kutazamwa na wapenda sinema.
Amesisitiza umuhimu wa kufurahia filamu hii na kuonyesha shukrani kwa wote waliohusika katika utengenezaji wake. Filamu hiyo inaweza kupatikana kwenye chaneli yake ya YouTube.