Sita kutoka Benki ya Akiba (ACB) wamejishindia zawadi za fedha taslimu na zawadi nyingine, baada ya kushiriki katika kampeni ya ‘Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari’. Hafla ya kukabidhi zawadi hizo ilifanyika tarehe 14 Februari 2025.
Akizungumza katika hafla hiyo, Ofisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank, Wezi Mwazani, alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja kutumia huduma za kidijitali kwa urahisi. Aliongeza kuwa huduma hizi zinaboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza usalama wa miamala.
Washindi walichaguliwa kulingana na matumizi yao bora ya huduma za kidijitali, zikiwemo ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card. Mwazani aliwashukuru washindi kwa kushiriki katika kampeni hiyo.
“Tunawapongeza washindi wetu kwa kuwa sehemu ya safari yetu ya kidijitali. Huduma kama ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card zinawasaidia wateja wetu kufanya miamala kwa haraka na salama. Tunawahamasisha wengine kuendelea kutumia huduma hizi kwa manufaa yao,” alisisitiza Wezi.
Washindi wa kampeni hiyo walionyesha furaha yao kwa kutambuliwa kwa matumizi yao ya huduma za kidijitali na waliahidi kuendelea kuzitumia zaidi. Kampeni ya ‘Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari’ ni sehemu ya mkakati wa Akiba Commercial Bank wa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kuwapa wateja wao ufumbuzi bora wa kibenki popote walipo.