JUMLA ya waogeleaji 14 wameunda timu ya Taifa kujiandaa na mashindano ya vijana ya kuogelea ya Afrika yatakayofanyika kuanzia Aprili 30 hadi Mei 3 mwaka huu nchini Misri.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa Chama cha Kuogelea Tanzania, timu hiyo imeshaanza maandalizi ya michuano hiyo kwa lengo la kushiriki kwa ufanisi.
“Kati ya waogeleaji hao, saba ni wanaume na saba ni wanawake. Uchaguzi wa kikosi umefanywa kwa kuzingatia mashindano mbalimbali yaliyopita, ikiwemo yale yaliyofanyika hivi karibuni,” alisema msemaji huyo.
Wao ni waogeleaji Romeo Mwaipasi, Aryan Bhatt, Mark Tibazarwa, Austin Okore, Christian Fernandes, Enrico Baretto, Sahal Haarunani, pamoja na Filbertha Demello, Lina Goyayi, Bridget Heep, Natalia Ladha, Amylia Chali, Aliyana Kachra na Aminaz Kachra.