Mbeya: Watu Watatu Wafariki Katika Ajali Kubwa, Wakiwemo Kiongozi na Mwandishi wa Habari
Watu watatu, akiwemo mwandishi wa habari wa kujitegemea, wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea mkoani Mbeya. Ajali hiyo, ilihusisha basi la kampuni ya CRN na gari la Serikali, na imesababisha pia majeruhi saba.
Ajali hii imetokea leo, Februari 25, 2025, katika eneo la Shamwengo wilayani Mbeya. Ilidaiwa kuwa basi lilikuwa likilipita gari la Serikali bila tahadhari, na kusababisha ajali iliyosababisha vifo hivyo na majeruhi kadhaa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa kati ya majeruhi saba, wawili wapo katika hali mahututi, wakati wengine wameachiliwa.
“Ejali hii imesababisha vifo vitatu, akiwemo mwandishi wa kujitegemea na wengine wawili. Tutaendelea kutoa taarifa kadri tunavyopata,” alisema Kamanda Siwa.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya, Christopher Uhagile, ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea wakati wakiwa na safari ya kumkamilisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Rajabu, aliyekuwa na ziara mkoani humo.
Uhagile amesema katika ajali hiyo, wamempoteza kiongozi Daniel Mselewa, ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa chama hicho, Wilaya ya Rungwe.
“Tayari CCM Taifa imeelekeza namna ya kuwasindikiza wapendwa wetu ambao ni marehemu, kwani walikuwa katika majukumu ya chama. Kesho tutangalia namna ya kufanya,” aliongeza Uhagile.
Endelea kufuatilia ECNETNews kwa habari zaidi kuhusu ajali hii na matukio mengine muhimu.