Benki ya CRDB yatangaza kampeni mpya ya SimBanking Humu Tu ikiwa na zawadi za fedha taslimu, magari, na simu janja kwa wateja. Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika leo, na lengo ni kuhamasisha matumizi ya huduma za SimBanking miongoni mwa jamii.
Kaimu Mkuu wa Biashara na Mkurugenzi wa uendeshaji matawi wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul, alieleza kuwa huduma za kisasa za benki zinaendana na mahitaji ya wateja, na benki inatumia teknolojia kubuni huduma mbalimbali. “Simbanking ni ‘Application’ ya kwanza kwenye soko letu, na imesaidia kuleta mapinduzi makubwa katika huduma za kifedha nchini Tanzania,” alisema Paul.
Simbanking ilianza mwaka 2011 na imewezesha Watanzania wengi kujiunga rasmi na mfumo wa kibenki, ikitoa huduma zinazopatikana masaa 24. Zaidi ya wateja milioni tatu tayari wanatumia Simbanking kufanya miamala kwa wakati wowote.
Kampeni ya Benki ni Simbanking Humu Tu itatoa zawadi mbalimbali kama magari mapya, Tembo Points, na Laptop mpya kwa wanafunzi wa vyuo. Kila baada ya miezi mitatu, kutakuwa na zawadi ya gari aina ya IST new model na Iphone 16 kwa wanafunzi, na mshindi wa jumla atapata Toyota Harrier New Model ifikapo Desemba.
Paul aliwataka wateja kufanya miamala kupitia App ya Simbanking au kwa kubonyeza 15003#. Mabalozi wa Benki ya CRDB, ikiwemo mwanamuziki Rayvan na Hamisa Mobeto, wamepongeza kampeni hiyo na kueleza umuhimu wa Watanzania kufungua akaunti ili kunufaika na fursa mbalimbali za Simbanking.