Rais Samia Suluhu Hassan amepokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award katika hafla iliyofanyika leo Februari 4, 2025, katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Tuzo hii inatambua viongozi ambao wametumia juhudi zao kuharakisha maendeleo ya kitaifa kuelekea malengo ya maendeleo endelevu. Rais Samia amepewa tuzo hii kwa mchango wake katika kupambana na vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano.