Kwa wagonjwa wa kisukari, kutumia chakula kama dawa ni mbinu muhimu ya kudhibiti ugonjwa huu na kupunguza madhara yanayoweza kutokea. Mlo sahihi ulio na viwango vya chini vya sukari unaweza kusaidia kuepusha matatizo yanayohusiana na kisukari.
Vyakula vyenye fiber kama matunda, mboga za majani, nafaka zis zokobolewa na wanga aina ya mizizi kama maboga ni muhimu kwa udhibiti wa viwango vya sukari. S pia, vyakula vya protini kama maharage na mbaazi vinapendekezwa.
Ulaji wa vyakula vya wanga asilia kama unga wa ngano, unga wa mahindi yasiyokobolewa, na shayiri vinaweza kusaidia kudhibiti sukari kwenye damu. Ni muhimu kuepuka vyakula vyenye sukari ya ziada kama keki na juisi za viwandani, kwani vinaweza kuharakisha ongezeko la viwango vya sukari.
Wagonjwa wa kisukari wanapaswa pia kuacha matumizi ya mafuta yanayotokana na wanyama na badala yake kutumia mafuta ya mimea, ikiwa ni pamoja na mafuta ya mizeituni, mafuta ya alizeti, na mafuta ya parachichi. Mafuta ya samaki na ubuyu yanajulikana kusaidia katika kudhibiti viwango vya sukari na kuboresha afya ya moyo.
Matunda na mboga za majani ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na fiber inayohitajika kwa udhibiti wa kisukari. Ingawa matunda yenye sukari ya asili kama tufaa na madalanzi yanaweza kuliwa, ni muhimu kuepuka matunda yanayoongeza sukari haraka kwenye damu kama vile zabibu na mananasi.
Kuhakikisha unanywa maji ya kutosha ni njia nyingine ya kudhibiti viwango vya sukari. Maji husaidia figo kufanya kazi vizuri katika kutoa sukari kwa njia ya mkojo, na pia husaidia kudhibiti uzito, jambo muhimu kwa wagonjwa wa kisukari.
Vyakula vyenye madini ya magnesium, kama mbegu za maboga, maharage, na spinach, vinachangia katika ufanisi wa insulin na udhibiti wa sukari.
Wagonjwa wa kisukari wanashauriwa kuwa makini na mlo wao, kufanya mazoezi mara kwa mara, kuepuka msongo wa mawazo, na kuhudhuria kliniki ya kisukari ili kusaidia katika kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu.