Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025, imetangaza kwamba tamasha hilo litafanyika katika mikoa 26 nchini Tanzania na kutafuta wadhamini wa kusaidia kufanikisha tukio hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, ilisema kuwa maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na kwamba litakazia uzinduzi wake katika Jiji la Dar es Salaam kabla ya kuendelea katika mikoa mingine nchini.
“Maandalizi ya tamasha yanaenda vizuri na tunakaribisha wadhamini kuunga mkono tukio hili kubwa litakalofanyika mikoa yote nchini Tanzania, tukianza na Mkoa wa Dar es Salaam,” ilisema kamati hiyo.
Wamesema kwamba kwa sasa wanajitahidi kuwasiliana na wafadhili, na ikiwa watafanikiwa kupata wadhamini, tamasha litakuwa bila kiingilio.
Tamasha la kuombea uchaguzi linatarajiwa kufanyika hivi karibuni na litaweka pamoja waimbaji wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.