Fainali ya shindano la kusaka vipaji nchini Bongo Star Search (BSS) inatarajiwa kufanyika Februari 28, 2025, katika Ukumbi wa Warehouse uliopo Masaki, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benchmark, Madam Rita Paulsen, ametangaza kwamba msimu wa 15 wa shindano hili umekuwa wa kipekee kwa kushirikisha washiriki kutoka Tanzania, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Madam Rita amesema, “Huu ni msimu wa tofauti kwa sababu tumefungua milango kwa Afrika Mashariki. Ushindani umekuwa mkubwa, lakini sasa tunakaribia kumpata mshindi.”
Aidha, ameeleza kuwa msanii Abiudi alijitoa kwenye mashindano kutokana na sababu binafsi zinazomhusu yeye na mpenzi wake.
Rita amewataka wadau wa muziki kuunga mkono jitihada za kusaidia vipaji chipukizi nchini.