Benki ya Akiba (ACB) yatoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Chakuwama kilichopo Sinza, Dar es Salaam.
Katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, alisema kuwa lengo ni kuboresha ustawi wa watoto na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao.
Amesema msaada huo, unaojumuisha mahitaji muhimu, unaonyesha dhamira ya benki kusaidia jamii na kujenga matumaini kwa mustakabali mwema. Akiba Commercial Bank inaamini katika nguvu ya mshikamano na kuleta mabadiliko chanya.
“Msaada huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha ustawi wa watoto hawa na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji kwa maisha bora yajayo,” alisema.
Mwakilishi wa kituo hicho alishukuru benki hiyo kwa ukarimu wao, akisema msaada huo utaleta mabadiliko katika maisha ya watoto hao.
“Tunawashukuru sana Benki ya Akiba kwa kutuunga mkono katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani, kutoa ni moyo,” alisisitiza.
Msaada huo utasaidia kukidhi mahitaji ya watoto na kuwapatia furaha, kupitia juhudi hizi, Benki ya Akiba inathibitisha dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii kwa vitendo, ikilenga kuleta mabadiliko chanya yanayodumu.