Baada ya muda mrefu kuwa kimya, mwongozaji na mwigizaji maarufu kutoka Houston, Texas, Alenga Elize, sasa anazindua filamu yake mpya ya Kiswahili inayoitwa Lost Love (Wolf in a Sheep’s Clothes).
Alenga, anayejulikana kwa uwezo wake wa kipekee katika tasnia ya filamu, ameendelea kuwakilisha kikamilifu filamu za Kiswahili nje ya mipaka ya Afrika, akijulikana kama mmoja wa viongozi wa tasnia ya Bondowood Movie Industry.
Akizungumza katika mahojiano, Alenga alifichua kuwa filamu hii mpya imepokelewa kwa furaha kubwa, na ndani ya kipindi kifupi, imefanikiwa kufikia watazamaji maelfu.
“Lost Love ni filamu yenye maudhui halisi ya Kiafrika. Inasimulia visa vya kusisimua, mapenzi halisi, na usaliti. Ni kazi ambayo haiwezi kukosekana. Natoa shukrani kwa timu yangu na waigizaji wote walioshiriki kuhakikisha filamu hii inakuwa bora,” alisema Alenga.
Filamu hiyo inaonyesha uwezo wa kipekee wa Alenga na timu yake katika kuleta simulizi zinazogusa maisha ya kila siku, huku wakichanganya utamaduni wa Kiafrika na hadithi zinazovutia kimataifa.
Alenga alisisitiza kwamba mafanikio ya kazi zake yanatia motisha ya kuendelea kukuza tasnia ya filamu ya Kiswahili akiwa ughaibuni.
Mashabiki wa filamu za Kiswahili wanakaribishwa kutazama Lost Love na kufurahia kazi hii iliyojawa na burudani na mafunzo kwa kila mmoja.