Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania imezindua promosheni maalumu kwa wateja na mawakala wake inayoitwa Airtel Santa Mizawadi katika kuelekea sikukuu.
Uzinduzi wa promosheni hiyo ulifanyika leo Desemba 17, 2024, katika makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, amesema promosheni hii inawawezesha washindi kupata zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na pocket WiFi, simu janja, pikipiki, luninga na fedha taslimi hadi shilingi milioni moja.
Mmbando alisisitiza kuwa Airtel Santa Mizawadi inatoa fursa kwa wateja na mawakala waaminifu kushiriki katika sherehe za sikukuu kwa kushinda zawadi ambazo zitaboresha maisha yao. “Kupitia promosheni hii, tunasambaza upendo na kunogesha sikukuu kwa wateja wetu ambao ni sehemu muhimu ya mafanikio yetu,” alisema.
Meneja Huduma kwa Wateja alisema kwamba Airtel inawathamini wateja wake na kuongeza kuwa promosheni hii itakuwa na faida kubwa kwao. “Mr SANTA wetu atakuwa akitembelea mitaa mbalimbali ili kutoa zawadi za papo kwa hapo kwa bahati. Hii ni fursa ya kipekee kwa wateja wetu,” alisema.
Washindi wa Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia droo zitakazochezwa kila wiki, ambapo wateja watajulishwa kupitia simu kwa nambari maalumu ya Airtel 100.
Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi; wakala wa Airtel anapaswa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, wakati wateja wanatakiwa kufanya miamala mbalimbali kama kununua bando, kutuma fedha, kulipa bili, na mengineyo kupitia nambari za huduma au ‘My Airtel App’.