Dar es Salaam, Tanzania
Bolt, kiongozi katika huduma za usafiri wa mtandaoni, sasa inathibitisha rasmi kuwa punguzo linalotolewa kwa abiria linagharamiwa kikamilifu na kampuni hii.
Taarifa hii inakuja kama majibu kwa dhana potofu kuhusu punguzo la safari zinazotolewa kwa abiria. Wengi wanaamini kwamba punguzo hizi zinaathiri mapato ya madereva, lakini Bolt inafafanua kuwa hali hii si sahihi.
“Abiria anapofaidika na punguzo kwenye nauli, Bolt hulipa dereva mara moja kwa kiasi kilichopunguzwa. Malipo haya huonyeshwa mara moja kwenye mapato ya dereva, kuhakikisha kuwa hakuna hasara ya kifedha inayopatikana. Mfumo huu umeundwa kwa uwazi ili madereva waweze kufuatilia mapato yao kwa urahisi kupitia programu ya Bolt,” alisema Meneja Mkuu wa Bolt Kenya na Tanzania.
“Ili kusaidia kuboresha uelewa, Bolt imeimarisha mawasiliano yake kati ya madereva na abiria. Kampuni inatoa taarifa za mara kwa mara kwa madereva kupitia arifa ndani ya programu, muhtasari wa mapato, na nyenzo za elimu kupitia SMS na barua pepe,” aliongeza.
Abiria wanahimizwa kulipa nauli inayoonyeshwa kwenye programu ya Bolt, bila ya kujadiliana au kulipa zaidi. Abiria wanaokutana na shinikizo kutoka kwa madereva kuhusu malalamiko ya punguzo wanatakiwa kuripoti matukio hayo kupitia programu ya Bolt.
Ripoti hizi zinasaidia Bolt kuchukua hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ziada kwa madereva au kusimamisha akaunti zao kwa ukiukwaji wa mara kwa mara. Kamisheni ya safari zenye punguzo huhesabiwa kwa kuzingatia gharama kamili ya safari kabla ya punguzo kutolewa, kuhakikisha madereva hawapotezi kipato chochote.
Pia, malipo yote ya punguzo hufanyika mara moja na yanaonekana katika mapato ya kila siku ya dereva, kuhakikisha uwazi na ufafanuzi wa mapato ndani ya programu ya Bolt.
Bolt inaendelea kujitolea kusaidia ustawi wa kifedha wa madereva, kutoa nauli za haki na nafuu kwa abiria, na kuimarisha uaminifu kati ya madereva na abiria kupitia mawasiliano bora.
Kampuni inaendelea kuboresha mfumo wa usafiri wa mtandaoni unaoaminika na wa haki, ambapo madereva na abiria wote wananufaika kutokana na huduma zinazotolewa.